• Malalamiko |
    • MAWASILIANO |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Wafanyakazi |
Kaliua District Council
Kaliua District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu, na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
      • Usafi wa Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Legal Unity
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Fursa za Uwekezaji

MKUU WA MKOA AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE NA KUKABIDHI HUNDI YA MILIONI 202 PAMOJA NA PIKIPIKI NANE MAAFISA MBALIMBALI

Posted on: October 21st, 2017

.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Ndugu Aggrey Mwanri amekabidhi vikundi vya wajasiriamali wilayani Kaliua hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 202.  Fedha hizo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani  ya Halmashauri ambapo 4% watapatiwa wanawake, 4% vijana na 2% walemavu.

Aidha Mkuu wa Mkoa kampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua Ndugu John Marco Pima kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kila mwezi wanatenga asilimia 10 ya mapato na kuiweka kwenye akaunti maalum.

Kwa upande mwingine mkuu wa mkoa amemtaka mkurugenzi mtendaji kuzingatia vigezo vya mikopo hiyo ikiwa ni pamoja na wakopaji kuwa katika  vikundi, wakopaji kujulikana makazi yao na shughuli zao za uzalishaji wanazozifanya. Mwanri amevitaka vikundi kurejesha mikopo yao kwa wakati na kwa utaratibu utakaowekwa ili waweze kukopesheka zaidi, vilevile amewataka wajasiriamali kutumia vyema mikopo yao badala ya kuzifanyia hanasa badala ya malengo yaliyokusudiwa na watumie faida itakayopatika kuimarisha hali za familia kiuchumi.

Aidha mkuu wa mkoa amezindua jukwaa la wanawake ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Raisi ambalo litasaidia kuinua hali za kiuchumi kwa wanawake wilayani Kaliua.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua alitangaza majina ya viongozi wa muda wa jukwaa kuwa; Mwenyekiti (Zainab Salum Andrea), Makamu Mwenyekiti (Teddy Mlekwa), Katibu (Anastazia Bebete), Katibu Msaidi (Mwajuma Mkwiti), Muweka Hazina (Bertha Samwel), Mjumbe (Joyce Springi). Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ameeleza kuwa jukwaa la wanawake litasaidia kutoa elimu, kurasimisha biashara ndogondogo, kukuza viwango vya bidhaa na kutoa mitaji na fursa za mitaji kwa wanawake.

Katika hafla hiyo Mh. Mwanri amekabidhi pikipiki nane kwa maafisa watendaji na maafisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Pikipiki nne zimekabidhiwa kwa maafisa watendaji na zingine zimekabidhiwa kwa maafisa ugani ili ziweze kuongeza tija kwa utendaji kazi wa watumishi hao na kusitiza kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Leo tunakabidhi pikipiki hizi kwa watumishi wachache lakini tutaendelea kuboresha kwa wengine kila tutakapopata fursa ya kufanya hivyo” Alisema Mkurugenzi Mtendaji.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI KALIUA DC MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II November 17, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • Ona zote

Habari za Hivipunde

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA WA MTAMBO DARAJA LA II {GREDA} NAFASI 01

    May 04, 2025
  • MNADA WA KWANZA WA ZAO LA KARANGA WILAYA YA KALIUA

    March 24, 2025
  • MADIWANI KALIUA WAPITISHA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA BAJETI YA BILION 50.2 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    January 30, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA KUPITIA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII IMETOA HUNDI YA TSH. 302,000,000/=

    December 23, 2024
  • Ona zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Kaliua 2018
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mwanzo
  • TAMISEMI
  • Huduma
  • Historia
  • Fursa za Uwekezaji
  • UTUMISHI

Kurasa zinazofanana

  • Salary Slips Portal
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya RC Tabora
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti za Serikali
  • Baraza la Mitihani - NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

MAWASILIANO

    Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni

    Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua

    Simu: +255262965676/9

    Dawati la Uwekezaji:

    Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz

Dawati la Malamiko

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Service

Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua