• Malalamiko |
    • MAWASILIANO |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Wafanyakazi |
Kaliua District Council
Kaliua District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu, na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
      • Usafi wa Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Legal Unity
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Fursa za Uwekezaji

HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA KUPITIA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII IMETOA HUNDI YA TSH. 302,000,000/=

Posted on: December 23rd, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mh. Dkt. khamis Mkanachi ambae amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.Paul Matiko Chacha kwenye Uzinduzi wa utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi kwa makundi Maalumu katika Halmashauri ya Wilaya ya kaliua katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri

Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vizuri Mapato ya ndani na kutoa asilimia kumi kwa Makundi maalumu kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya chama cha Mapinduzi.

‘’Jumla ya fedha iliyotengwa ya kiasi cha shilingi Bilioni moja na milioni mia mbili kwaajili ya mikopo hii ya asilimia kumi kwa awamu hii ya kwanza Milioni mia tatu na mbili ni sehemu ya Fedha inayokwenda kuwanufaisha wanufaika wa mikopo hiyo ambao ni Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu’’

Dkt. Khamis ameendelea kusema fedha hizi za mikopo zimekuja zikawasaidie watanzania kwani huu ndio mpango na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenda kuwasaidia Wananchi na kubadili maisha yao.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Jafael Lufungija amewaomba Wananchi kuendelea kuwa wazalendo katika ulipaji wa Tozo ambazo Halmashauri imeidhinisha katika maeneo ya Wilaya yetu

‘’Tukiona mtu anakwepa kulipa tozo tumuone ni sababu itakayo tupelekea tuikose ile asilimia kumi kutoka Mapato ya ndani kwa maana ya asilimia nne kwa Vijana, asilimia nne kwa Wanawake pamoja na asilimia mbili kwa Watu wenye mahitaji maalumu’’

Kwa awamu hii ya kwanza Jumla ya Vikundi 10 vimepokea hundi hiyo ikiwa ni Vikundi 7 kwa Wanawake na Vikundi 3 kwa Vijana.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI KALIUA DC MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II November 17, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • Ona zote

Habari za Hivipunde

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA WA MTAMBO DARAJA LA II {GREDA} NAFASI 01

    May 04, 2025
  • MNADA WA KWANZA WA ZAO LA KARANGA WILAYA YA KALIUA

    March 24, 2025
  • MADIWANI KALIUA WAPITISHA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA BAJETI YA BILION 50.2 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    January 30, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA KUPITIA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII IMETOA HUNDI YA TSH. 302,000,000/=

    December 23, 2024
  • Ona zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Kaliua 2018
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mwanzo
  • TAMISEMI
  • Huduma
  • Historia
  • Fursa za Uwekezaji
  • UTUMISHI

Kurasa zinazofanana

  • Salary Slips Portal
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya RC Tabora
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti za Serikali
  • Baraza la Mitihani - NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

MAWASILIANO

    Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni

    Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua

    Simu: +255262965676/9

    Dawati la Uwekezaji:

    Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz

Dawati la Malamiko

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Service

Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua